NAOT

MAADILI NA OFISI YA TAIFA YA UKAGUZI

Kwa mara ya kwanza mwaka huu 2016 Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali (NAOT) itashiriki katika maadhimisho ya Siku ya Maadili kitaifa. Ofisi hii ni miongoni mwa taasisi za Serikali zilizoanzishwa na katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara 143 ya mwaka 1977 yenye jukumu la kukagua na kutoa ripoti kuhusu mapato na matumizi ya rasilimali za umma.

Watanzania wengi tumekuwa tukijadili suala la maadili na uwajibikaji katika sura na mitazamo tofauti. Ni ukweli usiopingika kuwa suala la maadili linatofautiana kati ya nchi na nchi, taasisi na taasisi, familia na familia na hata rika. Hata hivyo licha ya tofauti hizi bado msingi ya maadili inafanana.

Miongozo ya utumishi wa umma nayo imetoa tafsiri kuhusu maadili. Aidha, Muongozo wa Ufafanuzi Kuhusu Maadili ya Utumishi wa Umma wa Mwaka 2007 umeetoa tafsiri ya maadili kwa kuunganisha maneno mawili ambayo ni neno, “maadili” na “msingi” na kisha kuja na tafsiri pana ambayo ni viwango vya utendaji vinavyokuongoza katika kufanya kilicho sahihi.

Muongozo unasisitiza kwamba, Maadili ya msingi yanawahusu wote, yaani yanakusudia kumwongoza kila mtu bila ya kujali hadhi yake katika jamii, umri, jinsia, dini au kabila. Ili nchi iwe na maendeieo ni muhimu kwa kila mwananchi kudhamiria kufikia kiwango cha juu cha uadilifu, Hii inamaanisha kwamba tunahitaji kufanya kilicho sahihi daima ili kujenga imani ya watoto wetu, watumishi wenzetu na wananchi wengine.

Taasisi zinazohusika na Maadili, Haki za Binadamu na Uwajibikaji ziliamua kufanya kampeni ya mwezi mmoja kuanzia tarehe 10 Novemba hadi 10 Desemba 2016. Katika kampeni hiyo pia waliandaa toleo maalum linaloonesha majukumu ya msingi ya kila taasisi, mafanikio na changamoto. Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi imeambatisha sehemu ya taarifa iliyochapishwa kwenye toleo hilo. Tafadhali pekua kiambatisho kupitia link hii.

 

Ijue Ofisi Ya CAG
Ijue Ofisi Ya CAG
Ijue-Ofisi-ya-CAG_4.pdf
761.8 KiB
2784 Downloads
Details...
2016

Comments are closed.