NAOT

CAG AFUNGUA WARSHA YA SIKU TATU KWA WATUMISHI WA OFISI ZA UKAGUZI AFRIKA MASHARIKI

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu Za Serikali Prof. Mussa J. Assad, amefungua Warsha ya Siku tatu kwa Wakaguzi wa kada ya Uhakiki wa Ubora kutoka Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi Tanzania, Kenya na Uganda.

Warsha hiyo yenye lengo la kuwajengea uwezo wakaguzi hao inayofanyika katika Hotel ya Protea Jijini Dar es salaam imeandaliwa na kufadhiliwa na Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi ya Sweden (SNAO).

Akifungua Warsha hiyo Prof. Assad, kwa pamoja amewataka washiriki hao kuhakikisha wanashiriki na kujifunza kwa bidiI ili kuleta tija na ufanisi zaidi katika utendaji kazi wao pindi watakaporudi katika maeneo yao ya kazi.

‘Najua mkitoka hapa hamtakuwa kama mlivyokuwa, nategemea mtakuwa tofauti zaidi baada ya kujengewa uwezo na wakufunzi kutoka ofisi ya Taifa ya Ukaguzi Sweden aliongeza’.

Katika Warsha hiyo yenye lengo la kuwajengea uwezo Wakaguzi hao wa kada ya Uhakiki wa Ubora pia watapata fursa ya  kubadilishana uzoefu juu ya utendaji bora zaidi wa kazi za Kikaguzi ili kuweza kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazojitokeza kila mara katika utendaji wa kazi zao za kikaguzi, uandaji wa ripoti za kikaguzi na utoaji na ufuatiliaji wa maoni ya kikaguzi.

2019

Comments are closed.