NAOT

Mchango wa Mhe. Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa Taasisi Simamizi katika kuimarisha Uadilifu, Uwazi Na Uwajibikaji nchini

Umuhimu na mchango wa utawala bora katika maendeleo endelevu ya

jamii na nchi kwa ujumla hauwezi kupuuzwa. Mwalimu Julius Kambarage

Nyerere alitufundisha “ili tuendelee tunahitaji mambo manne ya msingi”,

ambapo mojawapo kati ya hayo ni uongozi bora ambayo ni hali ya

kusimamia utekelezaji wa majukumu ya Serikali kwa kuzingatia misingi ya

utawala bora ambayo ni pamoja na uwazi, uadilifu, usikivu na uwajibikaji.

Aidha ili misingi hiyo iweze kutekelezeka zimeanzishwa taasisi za kusimamia

utekelezaji wake ambazo ni pamoja na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu

wa Hesabu za Serikali (NAO), Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma

(ES), Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Mamlaka ya

Usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bodi ya Taifa ya Wahasibu

na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa

Umma (PPRA). Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali (IAGD) na Mhasibu

Mkuu wa Serikali (ACCGEN).

Taasisi hizi pamoja na nyingine zenye majukumu yanayofanana na haya

zina wajibu wa kuhakikisha kuwa viongozi wa umma, watumishi wa umma

na taasisi zote za Serikali zinatimiza wajibu wao wa kuwaletea wananchi

maendeleo na kuzingatia uwazi na uadilifu katika maamuzi yanayofanywa

kwa niaba ya Serikali ikiwa ni pamoja na kusikiliza shida za wananchi na

kuzitafutia ufumbuzi stahiki.

Hata hivyo ili kufanikisha azma hiyo, Taasisi Simamizi zinahitaji uhuru katika

kutekeleza majukumu yake na kuwa na uwezo wa kutosha wa kusimamia

misingi hiyo. Hii inawezekana tu pale kunapokuwepo utashi wa kisiasa wa

kusimamia masuala hayo. Ni ukweli usiopingika kwamba Serikali ya Awamu

ya Nne chini ya uongozi wa Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete imekuwa na

utashi wa kisiasa, nia na dhamiri ya dhati katika kuhakikisha kuwa kuna

uwajibikaji, uwazi, uadilifu na usikivu katika uendeshaji wa shughuli za

Serikali. Kwa kuzingatia haya,Taasisi Simamizi zimewezeshwa kusimamia

masuala hayo.

Ni kutokana na ukweli huo, Taasisi zetu zimeamua kuutambua na kuuenzi

mchango wa Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya

Muungano wa Tanzania katika kuziwezesha Taasisi Simamizi kuimarisha

uwajibikaji, uwazi, uadilifu na usikivu Tanzania kwa lengo la kustawisha

maisha ya wananchi. Kutokana na hilo taasisi zetu zimeandaa kitabu

hiki chenye ujumbe juu ya ‘Kutambua jitihada za Serikali ya Awamu ya

Nne katika kuziwezesha Taasisi Simamizi kuimarisha uwazi, uadilifu na

uwajibikaji kwa lengo la kustawisha maisha ya wananchi’. Ni imani yetu

kuwa kupitia kitabu hiki utaungana nasi kutambua jitihada hizo.

Ahsante.

Ludovick S. L. Utouh

Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Viongozi wa Taasisi Simamizi

Juni 2014

KITABU CHA MCHANGO WA MHE. RAIS DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE KWA TAASISI SIMAMIZI KATIKA KUIMARISHA UADILIFU, UWAZI NA UWAJIBIKAJI NCHINI
2.4 MiB
1524 Downloads
Details...
2014

Comments are closed.