NAOT

Tanzania yakabidhi Ujumbe wake kwa Nchi ya Chile wakati wa Kikao cha 72 cha Bodi ya Ukaguzi wa Umoja wa Mataifa

 

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu (CAG)  za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Prof. Mussa Juma Assad amakabidhi nafasi yake ya Ujumbe wa Bodi ya Ukaguzi ya Umoja wa Mataifa (UNBoA) kwa nchi ya Jamhuri ya Chile alipohudhuria kikao cha 72 cha Bodi ya Ukaguzi ya Umoja wa Mataifa.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya makabidhiano yaliyofanyika kwenye Jengo la Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa (UN) tarehe 24 Julai, 2018 jijini New York nchini Marekani, Prof. Assad amesema kikao hicho ni cha mwisho kwa nchi ya Tanzania kuhudhuria kama Mjumbe wa Bodi ya UNBoA.

Prof. Assad amefafanua kuwa Tanzania itaendelea kuwa Tanzania itaendelea kuwa mjumbe mwangalizi “Observer Member” kwenye Jopo la Wakaguzi wa Nje wa Umoja wa Mataifa kwa kipindi cha miaka miwili mfululizo kuanzia tarehe 1 Julai, 2018. Pichani ni CAG Prof. Assad (watatu kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na maafisa alioambatana nao kwenye kikao hicho.

 

2018

Comments are closed.