NAOT

CAG AHUDHURIA HAFLA YA KUWEKA SAINI RIPOTI ZA UKAGUZI WA TAASISI ZA UMOJA WA MATAIFA

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Prof. Mussa Assad amehudhuria hafla ya kutia saini ripoti ishirini na nane (28) za Ukaguzi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa iliyofanyika tarehe 24 Julai, 2018 jijini New York nchini Marekani kwenye Ukumbi wa Mikutano uliopo katika Jengo la Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa (UN).

Hafla hii iliyofanyika wakati wa Kikao cha 72 cha Bodi ya Ukaguzi ya Umoja wa Mataifa (UNBoA) ilihudhuriwa na Wakaguzi Wakuu wa Hesabu za Serikali watatu ambao walitia saini kwa pamoja kwenye ripoti hizo. Wakaguzi Wakuu waliosaini ripoti za ukaguzi wa Taasisi za Umoja wa Mataifa ni pamoja na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali wa India Bw. Rajiv Mehrishi, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Prof. Mussa Juma Assad pamoja na Rais wa Taasisi Kuu ya Ukaguzi Ujerumani Bw. Kay Sceller.

Pichani ni  Bw. Rajiv Mehrishi (wa kwanza kulia),  Prof. Mussa Juma Assad (katikati) Bw. Kay Sceller (wa kwanza kushoto) wakitia saini kwenye kikao hicho.

2018

Comments are closed.