NAOT

TANZANIA KUWA MJUMBE MWANGALIZI KWENYE JOPO LA WAKAGUZI WA NJE WA UMOJA WA MATAIFA

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Prof. Mussa Assad amehudhuria kikao cha 72 cha Bodi ya Ukaguzi ya Umoja wa Mataifa (UNBoA) kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano uliopo kwenye Jengo la Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa (UN) tarehe 24 Julai, 2018 jijini New York nchini Marekani na kukabidhi nafasi yake ya Ujumbe wa Bodi ya Ukaguzi ya Umoja wa Mataifa (UNBoA) kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya Chile Bw. Jorge Bermudez Soto.

Akizungumza na waandishi wa habari waliohudhuria kwenye hafla hiyo ya makabidhiano Prof. Assad amesema baada ya Tanzania kumaliza kipindi chake cha kuwa Mjumbe na Mkaguzi wa Umoja wa Mataifa kwa kipindi cha miaka sita sasa Ofisi itakuwa Mjumbe Mwangalizi “Observer Member” kwenye Jopo la Wakaguzi wa Nje wa Umoja wa Mataifa. Pichani ni Prof. Assad (kushoto) akimpa mkono Bw. Soto baada ya makabidhiano. Katikati ni Mwenyekiti wa UNBoA na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali wa India Bw. Rajiv Mehrishi akishuhudia makabidhiano hayo.

2018

Comments are closed.