NAOT

Tanzania yashinda tuzo ya ripoti bora ya ukaguzi wa ufanisi

Shirika la Umoja wa Ofisi za Taifa za Ukaguzi Afrika (AFROSAI-E) leo limetoa tuzo kwa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (NAOT) kwa kushindanishwa na kuibuka mshindi wa kwanza katika ripoti bora ya mwaka 2016. Shindano hili linalosimamiwa na Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi ya Sweden iliwasilishwa kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa Bodi ya Wakaguzi Wakuu uliofanyika nchini Kenya mwezi huu Mei, 2017.

Tuzo hizi zimekuwa zikitolewa kila mwaka tangu mwaka 2008 ambapo tangu kuanzishwa kwa mashindano haya, Tanzania inashika ubingwa kwa mara ya pili.

Ripoti iliyoshinda kwa mwaka huu iliandikwa na timu ya wakaguzi watatu ambao ni Januari K. Kidunda, Asnath Mugasa na Yuster Salala.

Ripoti hiyo ya Ukaguzi wa Ufanisi imejikita katika kuangalia “Udhibiti wa Usafi Katika Maeneo ya Machinjio,” eneo ambalo ni la muhimu kwa umma wa Tanzania”.

Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi ni Taasisi Kuu ya Ukaguzi wa Umma ambayo mamlaka yake ni ya kikatiba kwa mujibu wa Ibara ya 143 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo yamefafanuliwa zaidi katika Sheria ya Ukaguzi ya Umma Na. ya Mwaka 2018.

2017

Comments are closed.