NAOT

UZINDUZI WA KAMPENI YA MAADHIMISHO YA KITAIFA YA SIKU YA MAADILI KUHUSU KUJENGA NA KUKUZA MAADILI, HAKI ZA BINADAMU, UWAJIBIKAJI, UTAWALA BORA NA MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA 10 NOVEMBA, 2016

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) mwaka huu alizindua Kampeni ya Kitaifa inayohusu Kujenga na Kukuza Maadili, Haki za Binadamu, Uwajibikaji, Utawala Bora na Mapambanao dhidi ya Rushwa. Uzinduzi huu ulifanyika  tarehe 10 Novemba, 2016 katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya TAKUKURU, Makao Makuu jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Maadili Kitaifa kwa mwaka 2016.

Wakati anazindua kampeni hiyo Mhe. Kairuki alisema “Kampeni hii ya mwezi mmoja ambayo itakuwa  endelevu imezinduliwa kwa lengo la kutafsiri kwa vitendo dhamira ya dhati ya Serikali ya Awamu ya Tano, inayoongozwa na Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kupiga vita vitendo vya rushwa, uzembe, ufisadi, matumizi mabaya ya fedha za umma, ukiukaji wa sheria, kanuni na taratibu ili kuimarisha misingi ya maadili, uwajibikaji na utawala bora nchini. Hivyo, Kampeni hii ya Kuhamasisha uzingatiaji wa Maadili, Haki za Binadamu, Utawala Bora na kuimarisha Mapambano Dhidi ya Rushwa ni mojawapo ya juhudi za Serikali za kuwahamasisha na kuwaelimisha wananchi kuikataa rushwa, kuwa waadilifu na kutambua haki zao.”

Shughuli nyingine zilizofanyika katika kipindi hicho cha kampeni ni Vipindi vya Elimu kwa Umma kupitia Vyombo vya Habari, Uchapishaji wa Makala Magazetini,  Midahalo, Matembezi ya Hiari na Kutoa  Huduma kwa Umma. Aidha, Siku ya Kilele cha  Maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za Binadamu ni tarehe 10 Desemba, 2016.

Taasisi hizo zilizoratibu kwa pamoja Maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za Binadamu ni ; Sekretariati ya Maadili ya Viongozi wa Umma (ES); Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU); Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora (POPSM); Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (NAOT); Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (CHRAGG); Tume ya Utumishi wa Umma (PSC) na Mamlaka ya Udhibiti wa  Manunuzi ya Umma (PPRA).

Mhe. Waziri alitoa wito kwa jamii nzima kuendelea kutumia fursa mbalimbali zitolewazo na Serikali kupata elimu kuhusu masuala ya Maadili, Haki za Binadamu, Uwajibikaji na Utawala Bora pamoja na kufahamu jitihada mbalimbali zinazofanywa na Serikali katika kudhibiti rushwa. Hotuba ya Waziri imeambatishwa.

UFUNGUZI KAMPENI YA MAADILI HOTUBA YA MHE  J  KAIRUKI
UFUNGUZI KAMPENI YA MAADILI HOTUBA YA MHE J KAIRUKI
UFUNGUZI-KAMPENI-YA-MAADILI-HOTUBA-YA-MHE.-J.-KAIRUKI_2.pdf
5.4 MiB
702 Downloads
Details...
2016

Comments are closed.