NAOT

WAJIBIKA: PIGA VITA RUSHWA, ZINGATIA MAADILI, HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA KUELEKEA UCHUMI WA KATI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, amezipongeza Taasisi saba zinazohusika na usimamizi wa Maadili, Haki za Binadamu, Uwajibikaji, Utawala Bora na Mapambano dhidi ya Rushwa kwa kazi nzuri wanayoendelea kuifanya katika kuhakikisha Utawala Bora na Maadili vinazingatiwa nchini.

Akizungumza kwenye hafla ya kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za Binadamu 2017 kilichofanyika kwenye viwanja vya Nyerere Square, mkoani Dodoma, Mhe. Makamu wa Rais amesisitiza Ajenda kubwa duniani kwa sasa ni kuhusu mapambano dhidi ya rushwa na kuimarisha Utawala Bora. Alifafanua kuwa Utawala Bora umebeba mambo muhimu kama Utawala wa Sheria, Haki za Binadamu, Maadili, uwazi na Uwajibikaji.

Aidha, Makamu wa Rais alisisitiza kuwa, Serikali imekusudia kuona nchi yetu inapata maendeleo kwa manufaa ya wananchi wake. Kufikia azma hii sio suala dogo ni lazima wananchi na Serikali kwa ujumla  kujidhatiti kutekeleza Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2025 pamoja na Ilani ya Uchaguzi ya Chama Tawala ya 2015/2020 inayolenga kuiwezesha nchi yetu kuwa ya Uchumi wa Kati unaoongozwa na viwanda. Hata hivyo alifafanua kuwa, juhudi za Serikali haziwezi kufanikiwa tusipodhibiti vitendo vya rushwa na kusimamia uadilifu na kuwajibika ipasavyo. Aliongeza kuwa Serikali itaendelea kuchukua hatua kwa wale wote watakaokwamisha kufikia azma hiyo.

2018

Comments are closed.