NAOT

TANZANIA YAMALIZA KIPINDI CHAKE CHA UJUMBE WA BODI YA UKAGUZI YA UMOJA WA MATAIFA

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Prof. Mussa Juma Assad amekabidhi nafasi yake ya ujumbe wa Bodi ya Ukaguzi ya Umoja wa Mataifa alipohudhuria kikao cha 72 cha Bodi hiyo kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano uliopo kwenye Jengo la Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa (UN) tarehe 24 Julai, 2018 jijini New York nchini Marekani.

Akizungumza na maafisa wake alioambatana nao kwenye kikao hicho Prof. Assad amesema Tanzania inakila sababu ya kujivunia kuingia katika historia ya dunia kwa kuwa nchi ya kwanza kwenye ukanda wa Afrika Mashariki na Kati kuteuliwa kuwa mkaguzi wa Umoja wa Mataifa kwa kipindi cha miaka sita. Prof. Assad amesisitiza kuhakikisha wakaguzi waliopata uzoefu na ujuzi mbalimbali kupitia fursa hiyo, wahakikishe wanautumia katika kuisaidia nchi yao. “Kama Taifa tunajivunia kuaminiwa na dunia kwa kupewa jukumu kubwa na nyeti lenye kuhitaji rasilimali watu wenye uweledi wa hali ya juu. Tumefanikiwa kuwajengea watumishi wetu uwezo ni lazima tuwatumikie watanzania wetu kwa kutumia uzoefu na ujuzi ulijengeka ili kulisaidia Taifa letu,” alisisitiza Prof. Assad. Pichani ni baadhi ya Ujumbe wa Tanzania ukifuatilia mada wakati wa Kikao cha 72 cha Bodi ya Ukaguzi ya Umoja wa Mataifa (UNBoA).

2018

Comments are closed.