NAOT

WANANCHI WATAKA SIKU ZA MAADHIMISHO YA UTUMISHI WA UMMA ZIONGEZWE

Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali (NAOT) imepokea maombi ya kuongeza siku za maadhimisho ya wiki ya utumishi wa umma, ili kutoa fursa kwa wananchi kukutana na maafisa wa Ofisi hii na kupata elimu kwa umma.

Akizungumza mmoja wa wananchi waliotembelea meza ya huduma iliyokuwa nje ya lango kuu la Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi – Makao Makuu jijini Dar es Salaam, amemuomba Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuwaruhusu watumishi wake kuendelea kutoa huduma  kwa wananchi kwa wiki mbili mfululizo ili kuwasaidia wananchi kufahamu majukumu ya Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi.

“Ni vyema huduma kama hii ikapewa muda wakutosha kuliko wiki moja. Wananchi wengi tunaogopa kuingia ndani ya jengo lakini mnapotoa huduma nje ya jengo inakuwa rahisi mno kwetu kuwafikia”, alisisitiza Moses Mbunda.

Katika kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma, kwa mwaka huu 2017 iliyoanza tarehe 16 na kumalizika tarehe 23 Juni, NAOT ilikutana na wananchi kwa ujumla kwa siku 7 kwa ajili ya kupokea na kuyatolea ufafanuzi malalamiko na kero za wananchi, kuhusu taarifa za ukaguzi na huduma zitolewazo kwenye Ofisi hii.

Zoezi hilo la kukutana na wadau lilitafanyika kati ya tarehe 19 na 30 Juni 2017, kuanzia saa 3.00 asubuhi hadi saa 11.00 jioni, katika Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi Makao Makuu, iliyopo mtaa wa Samora Machel/ Ohio, Jijini Dar es Salaam.

Aidha, baada ya maadhimisho hayo wadau walielekezwa kufika katika ofisi za NAOT kitengo cha Mawasiliano Serikalini, kutoa mrejesho au kuwasilisha kero zao.

2017

Comments are closed.