Ofisi yaTaifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali (NAOT), ikishirikiana na Shirika la maendeleo la Marekani USAID imefanya warsha yasiku moja na Waandishi wa Habari, Maafisa Habari, Wahariri, na Asasi za Kiraia yenye lengo la kukuza uelewa kuhusu ripoti za mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali itakayosaidia kupunguza upotoshaji wa nukuu za ripoti ili kufanikisha mjadala wa masuala ya taarifa za ukaguzi kufanyika kwa usahihi zaidi.

Warsha hiyo ya siku moja iliyofanyika Landmark beach hoteli jijini Dar es Salaam, ililenga kuwapa ufahamu juu ya uelewa wa ripoti za CAG na utekelezaji wa mapendekezo ya ripoti hizo.

Warsha hii inalenga kutoa fursa ya pekee kwa wadau wa NAOT kuweza kushiriki na kutoa mawazo ya namna ya kuboresha mawasiliano kati ya ofisi yaTaifa ya Ukaguzi na Wadau wake wakiwemo vyombo vya habari na asasi za kiraia.

“Lazima tufikirie  ni kitu gani kinatakiwa kuhusu mahusiano bora kati yetu, pia tutafakari ni kitu gani kinafaa zaidi kwa ujenzi wa nchi yetu ya Tanzania, Lazima pia tuelewe madhara ya yale tunayoripoti kwa upotoshaji na mipaka ya yale tunayoweza kuhitaji kuyaripoti’ ‘Bilashaka wote tunatambua umuhimu wa habari katika kuimarisha uwajibikaji na utawala bora ndani ya nchi yetu hivyo jukumu kubwa tulilonalo ni kutekeleza haki ya kikatiba na ya wananchi wa Tanzania katika kupata taarifa za utekelezajiwa sera, mipango na miradi mbalimbali ya maendeleo inayosimamiwa na Serikali.”

Bila kujua mahitaji ya wanahabari, Wahariri na wawakilishi wa Asasi za Kiraia, wadau wa ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali haitaweza kufikia malengo yake iliyojiwekea katika kuimarisha mahusiano yake, na wadau wake kwasababu wadau hao ambao ni muhimu kwa kuuelimisha umma kuhusu taarifa sahihi za matumizi ya rasilimali zao.

Kwa ujumla warsha hii itasaidia vyombo vya Habari kufahamu kwa upana kwa kuzingatia uwiano uliopo katika kutoa habari kwa wananchi kwa usahihi na kulinda haki za serikali ya kuzuia habari zisizo rasmi kama habari za uchunguzi, nakaguzi maalum ili kutoa taarifa sahihi za ukaguzi ili kupunguza upotoshaji nakufanikisha mjadala wa masuala ya ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.