Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Charles Edward Kichere leo tarehe 28 Machi, 2021 amemkabidhi Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ripoti za ukaguzi kwa mwaka wa fedha unaoishia tarehe 30 Juni 2020 katika halfa fupi iliyofanyika Ikulu Chamwino Jijini Dodoma na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali kutoka Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi.

Kwa Mujibu wa Ibara ya 143 kifungu kidogo 2 na 4 cha Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 (kama ilivyorekebishwa) kinamtaka Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kukabidhi Ripoti kwa Mheshimiwa Rais kabla au ifikapo tarehe 31 Machi kila mwaka na baada ya hapo Ripoti hizo huwasilishwa Bungeni ndani ya siku saba za mwanzo za kikao cha Bunge kinachofuata.