Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali  inaendesha warsha ya siku mbili (Februari 6-7,2020) kwa Wahariri wa vyombo vya Habari  na waandishi wa Habari  Mkoani Morogoro. Warsha hii ina lengo la kuwajengea Washiriki uwezo katika kuripoti taarifa za ubadhilifu zinazotokana na ripoti za ukaguzi zinazotolewa na ofisi hiyo.

Ofisi ina amini mafunzo haya yatasaidia kuviwezesha vyombo vya habari  kufikisha kwa Umma taarifa zinazohusu ripoti za kikaguzi zinazotolewa na CAG zinawafikia wananchi kwa usahihi kama zinavyotakiwa.

Warsha hii inafadhiliwa na programu kujenga uwezo endelevu wa Kupambana na Rushwa Tanzania (Building Sustainable Anti- Corruption Action Tanzania (BSAAT) ambayo ofisi inashiriki katika utekelezaji wake.Taasisi nyingine zinazoshiriki ni Wizara ya Katiba na Sheria,Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu,Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Sekretariati ya Maadili ya Viongozi,Ofisi ya Msajili wa Leseni na Biashara,Ofisi ya Utawala Bora na Maboresho na Mahakama.

Moja ya lengo la programu ni kuwajengea uwezo Watumishi wa ndani wa ofisi na Watumishi wa  sekta zingine za umma  pamoja na Wadau mbalimbali ikiwemo waandishi wa habari.

Pia programu hiyo inalengo la kujenga mfumo thabiti wa udhibiti wa rushwa, Kupitia na kuhuisha nyaraka mbalimbali na Kuboresha mazingira ya utendaji kazi ili kudhibiti rushwa ikiwa pamoja na Ufuatiliaji wa utekelezaji na kufuata miongozo mbalimbali  iliyoandaliwa.

Programu hii ya BSAAT inafadhiliwa na Serikali ya Uingereza/Northen Ireland kupitia Shirika lake la Maendeleo (DFID) pamoja na  Umoja wa Ulaya (EU)  kwa ajili ya utekelezaji.

Program hii ya miaka mitano ilianza kutekelezwa rasmi mwezi Septemba, 2018 na itaendelea mpaka mwaka 2013. Usimamizi na uratibu wa mradi huu upo chini ya  Ofisi ya Rais Ikulu.