Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi inaendesha kikao kikao kazi juu ya matumizi ya Nyaraka za Ukaguzi katika uchunguzi na uendeshaji wa mashauri Mahakamani yanayowashirikisha wataalamu kutoka Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi, TAKUKURU,Polisi,Mwendesha Mashtaka,Mwanasheria mkuu na Wakili Mkuu wa Serikali.

Mgeni Rasmi wa Kikao kazi hiki ni Mwakilishi wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ambaye ni Afisa Masuuli, Bwana Omary Mkomwa akifungua mafunzo hayo alisema, lengo kuu la kuwakutanisha wadau hawa ni kujenga mahusiano kati ya wadau ili kuboresha kazi za taasisi hizi. Pia inalenga kuwajengea wadau uelewa juu ya Masuala ya Ukaguzi na kuzungumzia namna bora zaidi ambayo taasisi na wadau wanaweza kutumia Taarifa za Ukaguzi kwa ajili ya uchunguzi na uendeshaji wa Mashauli Mahakamani.

Katika hatua nyingine, aliwashukuru shughuli hii kwa kukutanisha wadau hawa. Kikao hii kimewezeshwa na Mradi wa kujenga Uwezo endelevu wa Kupambana na Rushwa (Building Sustainable Anti-Corruption Action in Tanzania (BSAAT) chini ya ufadhadhili wa Serikali ya Uingereza/Northen Ireland kupitia Shirika lake la Maendeleo (DFID) pamoja na Umoja wa Ulaya (EU). Program hii ya miaka mitano ilianza kutekelezwa rasmi mwezi Septemba, 2018 na itaendelea mpaka mwaka 2023. Usimamizi na uratibu wa mradi huu upo chini ya Ofisi ya Rais Ikulu.

Alimaliza kwa kusema kutoa ushirikiano wa kutosha katika mafunzo hayo ili waweze kufikia malengo na kiujifunza mengi kutoka kwa kila mshiriki.