QR Code: ZGb8gjpVwv
Sehemu hii inatoa muhtasari wa ukaguzi uliofanyika kwenye miradi ya maendeleo nchini Tanzania kwa mwaka wa fedha 2023/24. Serikali ilitenga bajeti kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mikubwa kama vile Reli ya Kisasa (SGR), Mradi wa Umeme wa Maji wa Julius Nyerere (JNHPP) na Awamu ya Pili ya Mradi wa Mabasi Yaendayo Kasi. Ukaguzi uliofanyika ulijumuisha ukaguzi wa kifedha, utii wa sheria na ukaguzi wa kiufundi. Kaguzi 332 za kifedha zilihusisha tathmini ya mifumo ya uhasibu, udhibiti wa ndani wa matumizi ya fedha na taarifa za kifedha. Kaguzi 12 za kiufundi 12 zililenga kwenye mipango, usanifu, ununuzi, masuala ya Afya, Usalama na Mazingira, pamoja na usimamizi wa mikataba katika sekta za usafirishaji, nishati, maji na elimu.
0 Maoni