QR Code: QHh0tyY1pM
Kaguzi 14 za ufanisi zilifanyika mwaka huu zikilenga maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na usimamizi wa huduma za vivuko, udhibiti wa mafuriko, usalama wa vyombo vya majini, tiba asili na mbadala, utoaji wa vyeti vya kuzaliwa na kufa, data za kijiosayansi katika sekta ya madini, utekelezaji wa mpango wa vijana katika kilimo (BBT-YIA), huduma za ugani kwa mifugo, huduma za hali ya hewa, matumizi ya mashine za stakabadhi za kielektroniki (EFDs), biashara ya kaboni, utekelezaji wa mpango wa kupambana na jangwa, matumizi ya TEHAMA kwenye taasisi za udhibiti, na ufanisi wa gharama za mifumo ya TEHAMA iliyoandaliwa na taasisi za umma. Ripoti hii imebainisha mapungufu ya pamoja, hitimisho na mapendekezo ya kuboresha utoaji wa huduma kwa umma.
0 Maoni