QR Code: 6ViDtofzlp

Sehemu hii inahusu matokeo ya kaguzi 217 za Mashirika ya Umma kwa mwaka wa fedha 2023/24. Ripoti imeangazia masuala muhimu ya kifedha, udhibiti wa ndani wa shughuli na utendaji kazi wa taasisi katika kutekeleza majukumu yao. Pia, ripoti imetathmini ufanisi wa taasisi za udhibiti, mamlaka za maji, taasisi za elimu ya juu, sekta ya madini na utalii, benki za serikali na uwekezaji wa taasisi hizo, na kutoa mapendekezo ya kuimarisha ufanisi wa utendaji na matumizi ya fedha za umma.