QR Code: hTW$@0kO3p

Ripoti hii inatoa matokeo ya hoja za ukaguzi zilizoibuliwa, hitimisho, na mapendekezo kulingana na ripoti 12 za ukaguzi wa ufanisi zilizofanyika kwa mwaka wa fedha 2021/22. Ukaguzi wa ufanisi ulihusisha mada mbalimbali, ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa SDGs nchini Tanzania, usimamizi wa uondoshaji wa magari ya serikali, usimamizi wa usindikaji na uongezaji thamani wa mazao ya kilimo, udhibiti wa makampuni binafsi yanayojihusisha na ugawaji na udhibiti wa viwanja vya ardhi, matengenezo ya uendeshaji wa miradi ya maji, usimamizi wa viumbe vamizi, udhibiti wa malipo yanayofanywa na NHIF kwa watoa huduma za afya walioidhinishwa, usimamizi wa mifumo ya TEHAMA serikalini, udhibiti wa vifaa vya mionzi, udhibiti wa vituo binafsi vya afya, usimamizi wa shughuli za utafiti na ubunifu, na usimamizi wa miradi ya uwekezaji inayotekelezwa na PSSF na NSSF.