QR Code: wHG8rx3uqN

Ripoti hii inajumuisha Ukaguzi wa hesabu za mashirika ya umma 200 mwaka wa fedha uliofanyika kwa mwa fedha 2020/21. Ripoti hii imeangazia masuala yote muhimu ya ukaguzi yaliyobainishwa katika mwaka huu yanayohusiana na taarifa za fedha za mashirika ya umma na taasisi zingine, udhibiti wa uendeshaji na ufanisi wa uendeshaji wa taasisi katika utekelezaji wa majukumu ambayo yameanzishwa. Pia inaonyesha ufanisi wa kiutendaji wa vyombo vya udhibiti, mamlaka za maji na usafi wa mazingira, taasisi za elimu ya juu, na tathmini kuhusu sekta ya madini, mafuta na gesi, sekta ya utalii, benki za serikali na taasisi zingine za fedha na uwekezaji unaofanywa na mashirika ya umma na taasisi zingine za umma. Pia ripoti hii inajumuisha masuala yaliyojitokeza katika kaguzi maalum sita zilizofanyika katika Mashirika mbalimbali ya umma kwa mwaka wa fedha 2020/21.