Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali

Kuteuliwa kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.

Kabla ya uhuru wa Tanganyika Ofisi ilifahamika kama Idara ya Ukaguzi ndani ya Tanganyika na Kiongozi wa Ofisi hiyo alitambulika kama Mkurugenzi wa Ukaguzi.  Mkurugenzi huyo aliteuliwa na Katibu wa Jimbo au Gavana Mkuu kwa maelekezo ya Katibu wa Jimbo kwa niaba ya Mfalme au Malkia wa Uingereza.

Mapema kabla ya Uhuru wa Tanganyika mwaka 1961 baada ya sheria ya Exchequer and Audit Ordinance ya mwaka 1961 jina la taasisi lilibadilishwa kutoka Idara ya Ukaguzi na kuwa   Idara ya Malipo na Ukaguzi (Exchequer and Audit Department), pia jina la Mkuu wa Taasisi lilibadilika kutoka Mkurugenzi wa Ukaguzi na kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.

Wakati wa uhuru mamlaka ya uteuzi wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali yalikuwa kwa Gavana kwa kuzingatia ushauri wa Waziri Mkuu wa Tanganyika wakati huo. Mwaka 1962 iliundwa Katiba ya Jamhuri ya Tanganyika ambayo pia ilitambua uwepo wa Ofisi. Katiba hiyo ilibadilisha Mamlaka ya uteuzi kutoka kwa Gavana na kuwa mwanzo  wa kuwepo kwa Mamlaka ya kikatiba ya Rais kumteua mkuu wa taasisi. Hata katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatambua mamlaka ya  Rais kumteua mkuu wa taasisi hii.

Orodha ya Wadhibiti na Wakaguzi Wakuu wa Hesabu za Serikali waliowahi kuongoza Taasisi hii

Mr. Charles E. Kichere - CAG wa Sasa

Mr. Charles E. Kichere

CAG: 2019 - Soma Zaidi

Mr. Charles E. Kichere

CAG: 2019 -

Mtaalamu wa Uhasibu  na Mhitimu wa Masomo ya sheria, Bw. Kichere alisoma elimu na kutunukiwa shahada ya Biashara na shahada ya Uzamili katika usimamizi wa Biashara katika Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam  na shahada ya kwanza ya sheria katika chuo  Chuo Kikuu cha Tumaini, Jijini Dar es Salaam.

Kabla ya kuteuliwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali tarehe 03 Mwezi Novemba 2019, Bw. Kichere alihudumu katika nafasi ya Katibu Tawala wa Mkoa wa  Njombe.

Alikuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania kuanzia Machi 2017 hadi Juni 2019.Kabla ya hapo alikuwa Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania kuanzia Novemba 2016 hadi Machi 2017.

Bw. Kichere amewahi kuwa mjumbe wa Bodi ya Benki ya CRDB Tanzania.Pia alihudumu katika nafasi ya Mhasibu Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS).

Kabla ya kujiunga na Utumishi wa umma, Bw. Kichere alikuwa katika sekta binafsi ambapo alikuwa  Mkaguzi wa ndani  katika kampuni ya majani ya chai ya Unilever nchini Kenya na Tanzania.

Amepokea wadhifa wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kutoka kwa Profesa Mussa Assad ambaye muda wake wa utumishi wa miaka mitano uliisha tarehe 04 mwezi Novemba 2019.

Prof. Mussa Juma Assad - CAG Mstaafu

Prof. Mussa Juma Assad

CAG: 2014 - 2019 Soma Zaidi

Prof. Mussa Juma Assad

CAG: 2014 - 2019

Prof. Mussa J. Assad aliteuliwa kuwa Mdhibiti na  Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 05, mwezi Novemba 2014 na kuhudumu katika nafasi hii mpaka tarehe 04, Novemba 2019 ambapo muda wake wa utumishi ulimalizika.

Kaba ya Uteuzi wake, alikuwa ni Professor Mshiriki katika shule ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akifundisha masomo ya shahada za kwanza, uzamili na uzamivu. Pia alikuwa akifanya utafiti na  ushauri. Alihudumu katika Bodi ya Taasisi za Umma na binafsi.

Professor alisoma na kutunukiwa shahada ya Uzamivu katika chuo kikuu cha Southampton Shahada ya Uzamili katika Udhibiti wa Fedha na Chuo Kikuu cha Dublin City, Astashahada ya Uhasibu  Chuo Kikuu cha Dublin na Shahada ya Biashara  (uhasibu) kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam.

Mr. Ludovick S. L. Utouh - CAG Mstaafu

Mr. Ludovick S. L. Utouh

CAG: 2006 - 2014 Soma Zaidi

Mr. Ludovick S. L. Utouh

CAG: 2006 - 2014

Bw. Ludovick.S.L. Utouh aliteuliwa kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mwaka 2006 na alihudumu katika nafasi hiyo kwa kipindi cha miaka nane  mpaka mwaka 2014 alipostaafu baada ya kufikisha umri wa kustaafu kwa lazima  kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali ambao ni miaka 65.

Wakati wa utumishi wake katika nafasi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alihudumu pia kama mwenyekiti wa Umoja wa Taasisi kuu za ukaguzi wa nchi zinazoongea kiingereza na kireno (AFROSAI-E) na alikuwa ni mjumbe wa Bodi ya ukaguzi ya Umoja wa Mataifa.

Anakumbukwa kama kiongozi aliyesimamia mabadiliko mengi chanya ya ofisi ya taifa ya ukaguzi ikiwemo kutungwa kwa sheria ya ukaguzi wa umma, 2008 na kanuni zake za mwaka 2009 pamoja na miongozo kadhaa ya kazi za ukaguzi.

Kabla ya uteuzi wake alikuwa ni Mtendaji Mkuu wa kwanza  wa Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi Tanzania na kwa sasa anaongoza Taasisi ya WAJIBU.

Mr. Thomas Kiama - CAG Mstaafu

Mr. Thomas Kiama

CAG: 1996 - 2005 Soma Zaidi

Mr. Thomas Kiama

CAG: 1996 - 2005

Samahani! Hakuna Taarifa Sehemu hii kwa Sasa!

Mr. Gordon. A. Hutchinson - CAG Mstaafu

Mr. Gordon. A. Hutchinson

CAG: 1964 - 1969 Soma Zaidi

Mr. Gordon. A. Hutchinson

CAG: 1964 - 1969

Samahani! Hakuna Taarifa Sehemu hii kwa Sasa!

Mr. Mohamed Aboud - CAG Mstaafu

Mr. Mohamed Aboud

CAG: 1969 - 1996 Soma Zaidi

Mr. Mohamed Aboud

CAG: 1969 - 1996

Samahani! Hakuna Taarifa Sehemu hii kwa Sasa!

Mr. R.W.A. McColl - CAG Mstaafu

Mr. R.W.A. McColl

CAG: 1961 to 1963 Soma Zaidi

Mr. R.W.A. McColl

CAG: 1961 to 1963

Samahani! Hakuna Taarifa Sehemu hii kwa Sasa!