Muundo wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi uliidhinishwa na Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 05th Novemba, 2018

Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali, ina Divisheni saba (7) na Vitengo kumi (10).

  • Divisheni hizo ni Divisheni ya Ukaguzi wa Serikali Kuu;
  • Divisheni ya Ukaguzi wa Serikali za Mitaa;
  • Divisheni ya Ukaguzi wa Mashirika ya Umma;
  • Divisheni ya Ukaguzi wa Ufanisi;
  • Divisheni ya Ukaguzi wa Hesabu za Taifa;
  • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu;
  • Divisheni ya Mipango, Ufuatiliaji na Tathimini.


Aidha, Vitengo vilivyopo ni pamoja na Kitengo cha Huduma za Kiufundi;

  • Kitengo cha Ukaguzi wa Kiuchunguzi;
  • Kitengo cha Uhakiki wa Ubora wa Ripoti za Ukaguzi;
  • Kitengo cha Usimamizi wa Viashiria Hatarishi,
  • Kitengo cha Huduma za Kisheria,
  • Kitengo cha Fedha na Uhasibu,
  • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani,
  • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano;
  • Kitengo cha Ununuzi na Ugavi; na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.

Muundo