Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Bw. Charles E Kichere akisaini Kitabu cha Heshima nchini Rwanda tarehe 30/9/2021 alipotembelea eneo la kumbukumbu ya mauaji ya kimbari (Genocide) ya mwaka 1994 dhidi ya Watutsi na Wahutu wenye msimamo wa wastani. Inakadiriwa kwamba watu milioni moja waliuawa katika mapigano hayo yaliyodumu takribani siku 100. Kushoto kwake ni Bw. Obadiah. R. Biraro ambaye ni Mkuguzi Mkuu wa Jamhuri ya Rwanda na kulia ni Inspekta Jenerali Ms.Kiyango Générose ambaye ni Mkaguzi Mkuu wa Jamhuri ya Burundi.

CAG alitembelea Makumbusho hayo baada ya kutoka kwenye ukaguzi wa Mradi wa Kufua Umeme wa Rusumo. Mradi huo wa umeme wa maji unaotengenezwa kwa pamoja na Serikali za Burundi, Rwanda na Tanzania unasimamiwa na Kampuni ya Umeme ya Rusumo (RPCL) na kaguliwa kwa ushirikiano wa Wakaguzi Wakuu wa Nchi zilizotajwa hapo juu.