Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Bi. Wendy Massoy amefunga mafunzo kwa Wakaguzi wa Ufanisi kutoka nchi za Tanzania, Kenya, Rwanda na Uganda. Wawezeshaji wa mafunzo hayo Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi ya Sweden (SNAO) wameishukuru  Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi Tanzania (NAOT) kwa kuwezesha mafunzo hayo kufanyika kwa ufanisi na kukidhi malengo yaliyokusudiwa. Mafunzo hayo yamefanyika kuanzia Aprili 22-25, jijini Arusha.