Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Bw. Salhina Mkumba (katikati), katika picha ya pamoja na washiriki wa warsha ya ISSAI 130 kuhusu maadili na muongozo wa kimataifa katika ukaguzi. Warsha iliyoandaliwa na INTOSAI Development Initiative na kufanyika Dodoma, Novemba 15, 2023, ilihudhuriwa na viongozi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi, ikiwemo Mwezeshaji kutoka IDI, Bw. Alain Memvuh na Naibu Mkaguzi Mkuu, Bw. Benja Majura.