Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Bwana Charles E. Kichere amefungua mafunzo ya siku mbili kwaajili ya kuwajengea uwezo Wabunge wa Kamati za kudumu za Hesabu za Serikali (PAC) na kamati ya kuhudumu ya Serikali za Mitaa (LAAC) katika Ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa Jijini Dodoma.

Katika ufunguzi wa Mafunzo hayo Bwana Kichere ameahidi   kuwapa ushirikiano wa kutosha wabunge hao ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi zaidi.

Miongoni mwa Washiriki wa Mafunzo hayo ni Mwenyekiti wa kamati ya Kudumu ya PAC Mheshiwa Naghenjwa Kaboyoka ambaye pia ameahidi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi na pia amewaomba wabunge wa kamati hizo kutumia mafunzo hayo kama fursa ili kujifunza zaidi kwa sababu wabunge wengi waliopo katika kamati hizo bado ni wageni.“Nawaomba mtumie fursa hii kujifunza kwa moyo mmoja”.

Baada ya mafunzo Haya Wabunge hao wakishirikiana na Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wanatarajiwa kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni sehemu ya mafunzo kwa vitendo.