Naibu Mkaguzi Mkuu, Bw. George Haule (kulia) akikabidhi kwa niaba ya CAG cheti cha kuhitimu mafunzo, kwa Bw. Isaya Jeremia wakati wa kufunga mafunzo ya kuwajengea uwezo wa mbinu za ukaguzi, Wasaidizi wa Mkaguzi Mkuu (AAG’s) na Wakaguzi Wakuu wa Nje (CEA’s) wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (NAOT). Mafunzo hayo yaliyoendeshwa kwa njia ya mtandao yaliandaliwa na Bodi na Taasisi ya Ukaguzi wa Mafunzo ya Korea Kusini (AITI na BAI) kwa ushirikiano na NAOT. Hafla ya kukabidhi vyeti kwa Wahitimu imefanyika Makao Makuu ya NAOT jijini Dodoma Ijumaa, Agosti 12, 2022. (Picha: Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-NAOT).