Naibu Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Bw. Salhina Mkumba (katikati waliokaa) akiwa na Mkurugenzi wa Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika wa Benki ya Dunia, Bw. Asad Alam (wa pili kushoto waliokaa) mara baada ya Asad na Ujumbe wake kutembelea Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi jijini Dodoma Septemba 29, 2022 kwa lengo la kujadili maeneo ya ushirikiano na Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi. Wengine katika picha ni Viongozi kutoka Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi na Benki ya Dunia. (Picha kwa hisani ya Kitengo cha Mawasiliano Serikalini).