Rais wa Mahakama ya Ukaguzi wa Hesabu ya Ufalme wa Saudi Arabia, Dkt. Husam Alangari na Ujumbe wake wamefanya ziara kwenye Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi Tanzania (NAOT) ambapo wamepata fursa ya kufanya kikao kifupi (courtesy meeting) na mwakilishi wa CAG, Naibu Mkaguzi Mkuu, Bw. George Haule pamoja na baadhi ya Maofisa wa NAOT.