Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali  anapenda kuvijulisha vyombo vya Habari  na Umma wa Watanzania kwamba leo Tarehe 6 Aprili 2020 taarifa zake za Ukaguzi kwa Mwaka wa Fedha ulioishia Tarehe 30 Juni 2019 zimewasilishwa  Bungeni.Taarifa hizo ni:

  1. Ripoti ya Serikali Kuu;
  2. Ripoti ya Mamlaka za Serikali za Mitaa;
  3. Ripoti ya Mashirika ya Umma
  4. Ripoti ya Miradi ya Maendeleo;
  5. Ripoti ya Ukaguzi wa Ufanisi;
  6. Ripoti ya Ukaguzi wa mifumo ya TEHAMA; na
  7.  Ripoti 12 za ukaguzi wa ufanisi zinazohusu sekta mbalimbali kama zilivyoainishwa kwenye Jedwali Na. 1.

    Jedwali Na. 1: Ripoti za Ufanisi za Kisekta

Na.

Jina la Ripoti

1.

Ukaguzi wa Ufanisi wa Usimamizi wa Makusanyo ya Mapato kutoka kwa Makampuni ya Simu

2.

Ukaguzi wa Ufanisi wa Usimamizi wa Upatikanaji wa Umeme na Uhakika wa Utoaji Huduma za Umeme

3.

Ukaguzi wa Ufanisi Kuhusu Ufuatiliaji na Utekelezaji wa Shughuli za Manunuzi ya Umma

4.

Ukaguzi wa Ufanisi katika Usimamizi wa Miradi ya Ujenzi wa Maghala na Vihenge vya Kutunzia Mazao

5.

Ukaguzi wa Ufanisi katika Usimamizi wa Shughuli za Kinga na  Chanjo

6.

Ukaguzi wa Ufanisi kwenye Ubora wa Shughuli za Ujenzi na Ukarabati wa Barabara za lami Mijini

7.

Ukaguzi wa Ufanisi katika Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa ya Mifugo

8.

Ukaguzi wa Ufanisi kwenye Utekelezaji wa Jitihada za Kitaifa za Kupambana na utakatishaji wa Fedha nchini

9.

Ukaguzi wa Ufanisi juu ya Ukusanyaji Mapato toka vyanzo vya ndani katika Mamlaka za Serikali za Mitaa

10.

Ukaguzi wa Ufanisi katika Usimamizi wa Utoaji Programu za Kuwajengea Uwezo Walimu – Kazini

11.

Ukaguzi wa Ufanisi kuhusu Upatikanaji usioridhisha wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi yenye ubora kwa Watanzania.

12.

Ripoti ya ufuatiliaji wa mapendekezo ya ukaguzi wa ufanisi yaliyotolewa mwaka 2016

 

IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI

OFISI YA TAIFA YA UKAGUZI