Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali anapenda kuvijulisha vyombo vya Habari na Umma wa Watanzania kwamba leo Tarehe 6 Aprili 2020 taarifa zake za Ukaguzi kwa Mwaka wa Fedha ulioishia Tarehe 30 Juni 2019 zimewasilishwa Bungeni.Taarifa hizo ni:
- Ripoti ya Serikali Kuu;
- Ripoti ya Mamlaka za Serikali za Mitaa;
- Ripoti ya Mashirika ya Umma
- Ripoti ya Miradi ya Maendeleo;
- Ripoti ya Ukaguzi wa Ufanisi;
- Ripoti ya Ukaguzi wa mifumo ya TEHAMA; na
- Ripoti 12 za ukaguzi wa ufanisi zinazohusu sekta mbalimbali kama zilivyoainishwa kwenye Jedwali Na. 1.
Jedwali Na. 1: Ripoti za Ufanisi za Kisekta
|
Na. |
Jina la Ripoti |
|---|---|
|
1. |
Ukaguzi wa Ufanisi wa Usimamizi wa Makusanyo ya Mapato kutoka kwa Makampuni ya Simu |
|
2. |
Ukaguzi wa Ufanisi wa Usimamizi wa Upatikanaji wa Umeme na Uhakika wa Utoaji Huduma za Umeme |
|
3. |
Ukaguzi wa Ufanisi Kuhusu Ufuatiliaji na Utekelezaji wa Shughuli za Manunuzi ya Umma |
|
4. |
Ukaguzi wa Ufanisi katika Usimamizi wa Miradi ya Ujenzi wa Maghala na Vihenge vya Kutunzia Mazao |
|
5. |
Ukaguzi wa Ufanisi katika Usimamizi wa Shughuli za Kinga na Chanjo |
|
6. |
Ukaguzi wa Ufanisi kwenye Ubora wa Shughuli za Ujenzi na Ukarabati wa Barabara za lami Mijini |
|
7. |
Ukaguzi wa Ufanisi katika Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa ya Mifugo |
|
8. |
Ukaguzi wa Ufanisi kwenye Utekelezaji wa Jitihada za Kitaifa za Kupambana na utakatishaji wa Fedha nchini |
|
9. |
Ukaguzi wa Ufanisi juu ya Ukusanyaji Mapato toka vyanzo vya ndani katika Mamlaka za Serikali za Mitaa |
|
10. |
Ukaguzi wa Ufanisi katika Usimamizi wa Utoaji Programu za Kuwajengea Uwezo Walimu – Kazini |
|
11. |
Ukaguzi wa Ufanisi kuhusu Upatikanaji usioridhisha wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi yenye ubora kwa Watanzania. |
|
12. |
Ripoti ya ufuatiliaji wa mapendekezo ya ukaguzi wa ufanisi yaliyotolewa mwaka 2016 |
IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
OFISI YA TAIFA YA UKAGUZI