Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mussa Azan Zungu amefunga mafunzo kwa Wabunge yaliyolenga kuwaongezea ujuzi wa kuchambua na kujadili ripoti za ukaguzi zinazotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Mafunzo hayo ambayo yamefanyika Mkoani Singida yamewahusisha Wabunge wa Kamati nne (4) za Kudumu za Bunge ambazo ni pamoja na Kamatiya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) pamoja na Kamati ya Bajeti.