Mpango Mkakati wa Ofisi wa miaka mitano (5) umeanza kutumika tangu tarehe 1 Julai, 2016 na utagemewa kufikia ukomo tarehe 30 Juni, 2021. Mpango Mkakati huu umezingatia masuala yaliyoianishwa kwenye Mkakati ulioishia Juni, 2016.

Pia umeandaliwa kwa kuzingatia mafanikio yaliyopatikana na katika Mpango Mkakati uliopita kwa ajili ya muendelezo na kuzingatia maeneo yaliyoainishwa kwa ajili ya maboresho.

Aidha, mbali na mafanikio yaliyoorodheshwa katika Mpango mkakati uliopita Ofisi haikuweza kuyafikia malengo yote yaliyopangwa. Kuna Changamoto ambazo Ofisi ilikumbana nazo ikiwa ni pamoja na kushindwa kuiwezesha Ofisi kufanya Ukaguzi wa Kisasa na kuwaendeleza Wakaguzi Kitaaluma.