Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi inawatangazia wadau wake wote na Watanzania kwa Ujumla, Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (NAOT) imehamia rasmi Makao Makuu ya Serikali jijini Dodoma kuanzia Tarehe 01 Augosti 2019.

Kutokana na Ofisi kuhamia Makao Makuu ya nchi, Uongozi wa Ofisi unawajulisha kuwa huduma ambazo hapo awali zilikuwa zinatolewa katika makao makuu ya Dares Salam hazitoathirika kutokana na mabadiliko hayo.

Makao Makuu ya Ofisi yatakuwa jijini Dodoma mtaa wa Hazina Barabara ya kuelekea chuo kikuu UDOM. Anuani ya Makao Makuu Mapya ya Ofisi itakuwa kama ifuatavyo.