Toleo hili kwa ajili ya wananchi limegawanyika katika sehemu kuu tisa. Taarifa za fedha zilizokaguliwa kwa hesabu zinazoishia tarehe 30 June 2018 pamoja na ukaguzi wa Ufanisi na ukaguzi wa Mifumo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.
Sura ya Kwanza: Sura hii inatoa maelezo ya utangulizi wa kitabu hiki, wajibu na majukumu ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, madaraka yake, dhima na dira ya ofisi, misingi ya uadilifu pamoja na ufafanuzi wa baadhi ya maneno yaliyotumika katika kitabu hiki.