Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali imefanya kongamano la siku mbili kwa vyombo vinavyohusu matumizi ya taarifa za ukaguzi wa uchunguzi ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa shughuli za mradi wa kuongeza  mapambano dhidi ya rushwa chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la DFID

Kongamano hilo lilihusisha maofisa wa ofisi ya mwanasheria Mkuu, Mahakama, PCCB, FIU, DPP  na DCI, lilifanyika Bagamoyo na kufunguliwa na Naibu Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Bwana Jasper Mero ambapo aliwataka washiriki wa kongamano hilo kusimamia uwajibikaji na utawala bora. Bwana Mero,  aliwataka maofisa hao kutumia vyema fursa ya mahusiano yao kisheria kuboresha utendaji kazi ili kurejesha  imani ya wananchi kwa serikali yao.

Bwana Mero alisema, lengo la mpango huo ni kuongeza ufanisi zaidi katika utekelezaji wa matakwa ya sheria za ukaguzi.”Kifungu 27 cha sheria ya Ukaguzi wa umma ya mwaka 2008, kama vilivyofanyiwa mabadiliko ya sheria No 10 ya mwaka 2010, inatakiwa wakaguzi wanaofanya kazi kwa niaba ya mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali mara tu wanapobaini kuwepo kwa viashiria vya ulaghai au kughushi au rushwa wanapokuwa wanafanya ukaguzi kutoa taarifa kwa Mdhibithi na Mkaguzi Mkuu juu ya suala hilo”