Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi imekamilisha zoezi la kushirikisha wadau wake katika kutoa maoni kuhusu mabadiliko ya vipaumbele katika Mpango Mkakati wake wa mwaka 2016/17 hadi 2020/21.

Akizungumza baada ya kufanya mikutano miwili na wadau kuhusu Mpango Mkakati huo, Mkurugenzi wa Mipango wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi amesema zoezi hili limekuwa na manufaa makubwa kwani mpango mkakati huu unalenga kuwahudumia wadau kwa miaka mitano hivyo maoni yaliyotolewa yatasaidia kuboresha utoaji wa huduma kwa kadri ya matarajio ya wadau wa Ofisi hii.

Miongoni mwa maeneo ambayo yamefanyiwa mabadiliko katika Mpango Mkakati wa Ofisi ya Taifa ni mabadiliko ya Dira na Dhima ya Ofisi, viapaumbele vya Ofisi na malengo ya Ofisi kwa miaka mitano ijayo.

Mikutano ya wadau iligawanywa kwa makundi matatu. Kundi la kwanza lilihusisha viongozi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi na watumishi walio chini yao; kundi la pili lilihusisha mkutano kati ya Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi na Kamati za Bunge za PAC, LAAC na BIC kundi kundi la tatu na la mwisho lilihusu Ofisi ya Taifa ya na wakaguliwa, vyombo vya habari, asasi za kirai, taasisi binafsi za ukaguzi, taasisi za elimu pamoja na wadau wa maendeleo.

Baada ya kupitia hatua hizo, ofisi inatarajia kuzindua Mpango Mkakati huu wa miaka mitano mwishoni mwa mwezi huu wa saba.