Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali anapenda kuutarifu Umma kuwa, Sheria ya Ukaguzi wa Umma, sura ya 418 imefanyiwa mapitio na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Sheria hii iliyopitiwa imeanza kutumika tangu ilipotangazwa katika Gazeti la Serikali namba 13 la tarehe 1 Januari mwaka 2021 na inajumuisha maboresho yote yaliyofanywa katika sheria hii hadi kufikia tarehe 30, Juni mwaka 2020.

Sheria hii inaweza kurejewa kama Sheria ya Ukaguzi wa Umma [Sura ya 418 Toleo la Mwaka 2020] na kwa kiingereza "The Public Audit Act[CAP 418 R.E. 2020]"

Kufungua sheria hiyo bofya hapa