QR Code: nup3JkseFO
Ripoti hii inahusu mwaka wa fedha 2024/25, ikijumuisha kaguzi za kifedha (financial audits) na kaguzi za kiufundi (technical audits) za miradi ya maendeleo inayofadhiliwa na Washirika wa Maendeleo na Serikali ya Tanzania (GoT).
Jumla ya kaguzi 331 ni za kifedha, na kaguzi saba (7) ni za kiufundi, zilizofanyika kwa kutumia mbinu za ukaguzi wa wakati halisi (real-time audit) katika miradi mikubwa ikiwemo miundombinu ya viwanja vya ndege, miundombinu ya michezo (AFCON 2027), Barabara ya Mzunguko ya Dodoma, BRT Awamu ya 3 na 4, Bandari ya Uvuvi Kilwa Masoko, Kituo cha Mafuta Bandari ya Dar es Salaam, miradi ya maji vijijini ya RUWASA, pamoja na mradi wa TACTIC.
Ripoti inaonesha kuwepo kwa udhaifu katika ununuzi wa umma, usimamizi wa mikataba, utekelezaji wa bajeti, na usimamizi wa miradi, hali inayoathiri utekelezaji kwa wakati na thamani ya fedha, pamoja na ucheleweshaji wa utekelezaji wa mapendekezo ya ukaguzi.
0 Maoni