QR Code: JT74ulfb92
Ripoti hii inawasilisha matokeo ya ukaguzi kwa taasisi 221 kwa mwaka wa fedha 2024/25, zinazojumuisha Mamlaka 184 za Serikali za Mitaa, Sekretarieti za Mikoa 26, taasisi tanzu 3, Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (PMO-RALG), taasisi 6 zilizo chini ya PMO-RALG, pamoja na Mfuko wa Barabara.
Ukaguzi ulijumuisha mapitio ya taarifa za kifedha, mifumo ya udhibiti wa ndani, na utekelezaji wa bajeti. Ripoti inaonesha maeneo muhimu yanayohitaji kuboreshwa, ikiwemo usimamizi wa mapato (ikiwemo makusanyo yasiyowekwa benki), udhaifu katika ununuzi wa umma, kasoro katika usimamizi wa mali (hasa uuzaji wa ardhi), uwekezaji wa mamlaka za serikali za mitaa, pamoja na utendaji wa Mfuko wa Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu (WYDF).
0 Maoni