QR Code: l7SsO35jnz

Ripoti hii inawasilisha matokeo ya ukaguzi kwa taasisi 562 za Serikali Kuu, zikiwemo Wizara, Idara, Wakala, Mfuko Mkuu wa Hazina, Balozi za Tanzania nje ya nchi, pamoja na Vyama vya Siasa.

Ripoti hii inachambua uandaaji na uwasilishaji wa taarifa za kifedha pamoja na uzingatiaji wa sheria na kanuni, na kutoa muhtasari wa masuala muhimu yanayohusu maandalizi na utekelezaji wa bajeti, utendaji wa ukusanyaji wa mapato ya ndani, usimamizi wa matumizi, deni la taifa, utawala wa manunuzi ya umma, na utoaji wa huduma katika sekta za kipaumbele kama afya, maji, na miundombinu.