QR Code: FaXrVIE2q7

Ripoti hii inaangazia matokeo ya ukaguzi na mapendekezo ambayo chimbuko lake ni ukaguzi wa taarifa za fedha na uzingatiaji wa Sheria, Kanuni, na Miongozo mbalimbali uliofanyika katika mamlaka 185 za serikali za mitaa katika Mikoa 26 ya Tanzania Bara kwa mwaka 2020/21. Ripoti hii inagusa masuala yote muhimu ya ukaguzi yaliyobainika katika ukaguzi wa taarifa za fedha na ufanisi wa kiutendaji ndani ya mamlaka za serikali za mitaa katika utekelezaji wa majukumu yao ya msingi. Masuala hayo ni kama  mapitio ya mifumo ya udhibiti wa ndani, mapitio ya bajeti na mapato hasa katika changamoto zinazozikabili mamlaka za serikali za mitaa katika kukusanya mapato na changamoto za mifumo ya mapato. Miongoni mwa maeneo mengine, taarifa hii pia imebainisha madhaifu katika usimamizi wa fedha zilizoidhinishwa kwa matumizi ya mamlaka hizo, rasilimali watu, na manunuzi. Pia inaoangazia tathmini ya ufanisi katika sekta ya elimu na afya, ufanisi katika uwekezaji unaofanywa na mamlaka za serikali za mitaa na uendeshaji wa Mfuko wa Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu. Kaguzi maalumu 37 zenye hadidu maalum za rejea ambapo muhtasari wa matokeo ya kaguzi hizo yamejumuishwa katika ripoti hii.