QR Code: GTfoI94iUz

Ripoti inahusisha taasisi zilizokaguliwa ikijumuisha mafungu 56, ambayo ni Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, pamoja na taasisi saba shiriki, ambazo ni Wakala wa Mabasi Yaendayo Kasi (DART), Taasisi ya Mafunzo ya Serikali za Mitaa (LGTI), Mfuko wa Barabara chini ya PO-RALG, Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa (LGLB), Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini Tanzania (TARURA), Chama cha Wenyeviti wa Serikali za Mitaa Tanzania (ALAT) na Fungu Na. 2 - Tume ya Huduma ya Walimu (TSC). Pia ilihusisha Sekretarieti za Mikoa 26 na Mamlaka za Serikali za Mitaa 184 na matawi mawili halmashauri ya Arusha Meat na Shirika la Maendeleo la Dar es Salaam (DDC), na kufanya jumla ya taasisi zilizokaguliwa kuwa 220.