Naibu Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Bw. Salhina Mkumba (watatu kushoto waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa NAOT kutoka Divisheni mbalimbali ambao wameshinda Tuzo ya CAG ya Ripoti Bora ya Ukaguzi kwa mwaka wa fedha 2020/2021. Mkumba amekabidhi zawadi hizo kwa niaba ya CAG kwa lengo la kuwaongezea motisha Wakaguzi ili waweze kuandaa Ripoti zenye ufanisi na ubora  kwa maslahi ya Taifa. Hafla ya kukabidhi zawadi hizo imefanyika siku ya Ijumaa, Septemba 9, 2022 katika Ofisi za NAOT jijini Dodoma.