Report Reference Number: Ripoti/Tehama/2020/21

QR Code: U96zxJC4FY

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali amekagua mifumo na uendeshaji wa TEHAMA katika mwaka wa fedha ulioishia tarehe 30 Juni 2021. Ripoti hii ya jumla inatoa muhtasari wa matokeo muhimu yaliyotokana na kaguzi 44 zilizofanywa ambazo ripoti zake za ukaguzi zimetolewa kwa taasisi zilizokaguliwa. Lengo kuu la ukaguzi wa Mifumo ya TEHAMA lilikuwa kubaini kama udhibiti wa ndani wa TEHAMA ulikuwa mzuri na wa kutosha ili kuhakikisha matumizi ya TEHAMA yanafikia lengo. Mambo mahususi ambayo yalilengwa na ukaguzi ni: kuhakiki kiwango cha uzingatiaji wa sheria, sera na viwango vinavyotumika kuhusiana na TEHAMA, kutathmini ukamilifu wa taarifa kutoka kwenye mifumo ya TEHAMA ambayo ina athari kwenye taarifa za fedha za taasisi, kuangalia kama kuna matukio ya uzembe katika matumizi na usimamizi wa mifumo ya TEHAMA, pamoja na kupata uhakika wa kama mifumo ya TEHAMA inalindwa vya kutosha ili kutoa taarifa za kuaminika kwa watumiaji.