QR Code: jNg9vEMUGZ

Ripoti hii inatoa muhtasari wa matokeo wa kaguzi 40 za mifumo ya TEHAMA zilizofanyika kwa mwaka wa fedha 2021/22, zinazojumuisha kaguzi 21 zinazojitegemea na 19 kama sehemu ya kaguzi za fedha. Lengo kuu la ukaguzi huu lilikuwa kubaini ikiwa udhibiti wa ndani wa TEHAMA ulikuwa na ufanisi wa kutosha kufikia malengo yaliyokusudiwa. Hasa, ukaguzi ulilenga kutathmini uzingatiaji wa sheria, sera, na viwango vinavyotakiwa kwatika TEHAMA, kutathmini ukamilifu wa taarifa kutoka kwenye mifumo ya TEHAMA ambao unaathiri taarifa za kifedha za taasisi, kuangalia kama kuna mapungufu katika matumizi na usimamizi wa mifumo ya TEHAMA, pamoja na kuthibitisha kama mifumo ya TEHAMA inalindwa vya kutosha ili kutoa taarifa za kuaminika kwa watumiaji.