QR Code: GYcMfC2pSV

Ripoti hii inawasilisha muhtasari wa ukaguzi uliofanyika katika miradi ya maendeleo nchini Tanzania katika mwaka wa fedha 2021/22. Serikali ilitenga bajeti ya kusaidia utekelezaji wa miradi ya maendeleo, ikiwemo miradi ya kimkakati kama vile Reli ya Standard Gauge (SGR), Mradi wa Umeme wa Maji Julius Nyerere (JNHPP), na ujenzi wa mwendokasi awamu ya Pili. Ripoti hiyo inahusu aina tatu za ukaguzi uliofanywa katika miradi ya maendeleo ambayo ni fedha, uzingatiaji sheria na ukaguzi wa kiufundi. Ukaguzi wa fedha ulitathmini mifumo ya fedha kihasibu, udhibiti wa ndani wa usimamizi wa fedha, na taarifa za fedha, na kupelekea ripoti 290 za ukaguzi na maoni yaliyotolewa kwa taasisi zilizokaguliwa. Ukaguzi wa kiufundi, ulijikita katika upangaji, usanifu, ununuzi, afya, usalama na Mazingira (HSE), na masuala ya usimamizi wa mikataba ya miradi ya ujenzi katika sekta za usafirishaji, nishati, maji na elimu, ambapo kaguzi 10 zilifanyika kwa jumla.