QR Code: ERsVw9iZkP

Ripoti hii inachambua matokeo, mapendekezo na mahitimisho katika ukaguzi wa taarifa za kifedha na utiifu wa Idara mbalimbali za Serikali, Mashirika, na Taasisi zingine kwa mwaka wa fedha ulioishia tarehe 30 Juni 2023. Ukaguzi ulijumuisha mafungu (Votes) 475 za Wizara, Idara na mawakala wa Serikali. Hii inajumuisha mafungu 64, balozi 43, Idara na mawakala wa Serikali 30, Mifuko Maalum 19, Vyama vya Siasa 19, Hospitali za Rufaa na Maalum 34, Taasisi Nyingine 266.