QR Code: 4b9ME@lSTf

Ripoti hii inatoa muhtasari wa matokeo ya ukaguzi kwa Mamlaka za Umma na Taasisi zingine (PA&OBs) katika mwaka wa fedha 2021/22. Jumla ya kaguzi 206 zilifanyika katika kwa mwaka huu, na ripoti hii inaangazia masuala muhimu ya ukaguzi yanayohusiana na taarifa za fedha za PA&OBs, udhibiti wa ndani, na  ufanisi wa taasisi katika kutimiza majukumu yake. Ripoti hii pia inatathmini ufanisi wa taasisi za udhibiti, mamlaka za maji, na taasisi za elimu ya juu, na sekta ya utalii, benki za serikali na taasisi nyingine za kifedha, na uwekezaji unaofanywa na PA&OBs. Kwa ujumla, ripoti hii inatoa maelezo kuhusu matokeo ya ukaguzi na mapendekezo ili kuboresha shughuli na ufanisi wa mashirika na taasisi zingine za umma.