QR Code: zS7aYekHE8

Kwa mwaka wa fedha 2020/21 Idadi ya taasisi za Serikali kuu nilizokagua ni 331. Ripoti inaangazia mambo muhimu yanayohusu taarifa za fedha za Serikali Kuu, udhibiti wa utendaji na ufanisi katika utendaji wa Taasisi katika kutekeleza majukumu ya uanzishwaji wao. Pia inelezea ufanisi katika utendaji wa Vyama vya Siasa. Ripoti hii pia inaangazia masuala yaliyojikeza katika ukaguzi wa awali wa majalada ya mafao kwa fedha zinazolipwa kutoka Mfuko Mkuu wa Serikali. Aidha, ripoti hii imejumuisha matokeo ya kaguzi 11 maalumu zilizoombwa na wadau mbalimbali na zile zilizoanzishwa na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha 2020/21.